Uchimbaji wa Visima vya Maji

Uchimbaji wa Visima vya Maji
  1. Uchimbaji wa Visima vya Maji (Borehole Drilling)

    • Mtambo huu hutoa huduma za kitaalamu za uchimbaji wa visima virefu na vifupi kwa matumizi ya taasisi, jamii, na watu binafsi katika maeneo mbalimbali nchini.

  2. Huduma za Upimaji wa Eneo (Site Surveying)

    • Kabla ya uchimbaji, wataalamu wa Magereza hufanya uchunguzi wa awali (geophysical survey) ili kubaini uwepo na kina cha maji ardhini.

  3. Ufungaji wa Pampu na Mfumo wa Usambazaji Maji (Pump Installation & Water System Setup)

    • Baada ya visima kuchimbwa, Shirika la Magereza hutoa huduma za kufunga pampu (manual au electric/solar) pamoja na miundombinu ya mabomba kwa usambazaji wa maji.

  4. Matengenezo na Ukarabati wa Visima (Maintenance & Rehabilitation)

    • Huduma ya ukarabati wa visima vilivyokauka au vilivyoharibika, ikijumuisha kubadilisha pampu, kusafisha visima na kurekebisha mfumo wa usafirishaji maji.

  5. Huduma za Ushauri wa Kiufundi (Technical Consultancy)

    • Shirika la Magereza pia hutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu mbinu bora za upatikanaji, usimamizi, na uhifadhi endelevu wa vyanzo vya maji.

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo