Shirika la Magereza lilianzishwa mwaka 1983 kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika Namba 23 ya mwaka 1974 (The Corporations Sole {Establishment} Act CAP119 R.E. 2002) pamoja na kanuni zake za Mwaka 1983 (The Corporation Sole {Prisons Department} Regulations GN 128 of 1983. Na marekebisho yake ya GN 179 ya 1983, GN 640 ya 1986 na GN 155 ya 2001.
Shirika ni chombo ndani ya Jeshi la Magereza kinachoweza kufanya Shughuli za uzalishaji kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1974. Tofauti na mashirika mengine ya umma Shirika hili linaendesha shughuli zake kiuchumi kwa njia ya kuzungusha mtaji wake wa ndani kufanya biashara.
Vilevile, Shirika lina jukumu la kurekebisha wafungwa (Urekebu) kupitia shughuli zinazofanyika kwenye miradi kwa kutoa stadi za kazi na ujuzi utakaowezesha kumbalisha tabia baada ya kutumikia kifungo.
Shirika linafanya kazi zake za uzalishaji kibiashara ili kusaidia serikali katika kuhudumia mahitaji ya kuendesha shughuli za Jeshi la Magereza kupitia faida itakayozalishwa na Shirika na kuchangia pato la serikali ktpitia kodi na tozo mbalimbali.