MAGEREZA NA WIZARA YA KILIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI
Imewekwa: 25 Mar, 2026
MAGEREZA NA WIZARA YA KILIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI

‎Kamishna wa Huduma za Urekebu wa Jeshi la Magereza (CP) Amina Kavirondo leo Machi 25, 2026 amefungua kikao cha mwendelezo wa mashirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Wizara ya Kilimo katika uzalishaji wa mazao na usalama wa chakula.

‎Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Magereza, CP Kavirondo amesema lengo la kikao hicho ni kujadili kwa kina namna bora ya kuboresha ushirikiano katika sekta ya kilimo ili kuongeza tija, kuimarisha mnyororo wa thamani na kufikia kujitosheleza kwa chakula ndani ya Jeshi la Magereza.

‎Pamoja na mambo mengine, ameongeza kuwa jitihada hizo zitasaidia kupunguza utegemezi wa Serikali katika kugharamia chakula cha magereza.

‎Kwa upande wake, Afisa Kilimo Mkuu Dkt. Abel Leonard Mtembeji, akimwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Masoko na Usalama wa Chakula, amepongeza ushirikiano huo na kusisitiza kuwa unalenga kuimarisha uzalishaji wa kilimo kulingana na mipango ya kukuza sekta hiyo kwa kufikia ukuaji wa hadi asilimia 10 ifikapo mwaka 2035 na dira ya maendeleo ya kilimo ya mwaka 2050.

ACP Abdallah Omari Msepwa, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika

 

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo