Imewekwa: 23 Dec, 2025
Leo tarehe 23/12/2025, Kampuni ya Ulinzi Shima Guard Company Ltd, ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Magereza (SHIMA), imefanya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi.
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, CP Chacha Bina, kikilenga kujadili masuala muhimu ya uendeshaji wa kampuni, mikakati ya kuimarisha huduma za ulinzi, pamoja na mwelekeo wa ukuaji na maendeleo ya Shima Guard Company Ltd. Uongozi wa kampuni umeendelea kusisitiza dhamira ya kutoa huduma bora, za kuaminika na zenye kuzingatia weledi kwa wateja wake.



