Imewekwa: 06 Jul, 2023
KAMISHNA wa Polisi Zanzibar Khamis Hamad Adam, leo Julai 06, 2023 ametembelea Banda la Magereza
katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yaliyoanza Juni 28, 2023 ambapo amepata
fursa ya kuangalia bidhaa mbalimbali zilizopo Ndani ya Banda letu.