Kamati ya Bunge yaridhishwa na hatua za Ujenzi za Ofisi za TAKUKURU kupitia Mkandalasi wake Shirika la Magereza (SHIMA)
Imewekwa: 14 Mar, 2024
Kamati ya Bunge yaridhishwa na hatua za Ujenzi za  Ofisi za TAKUKURU kupitia Mkandalasi wake  Shirika la Magereza (SHIMA)

Kamati ya Bunge Yaridhishwa na hatua za Ujenzi za  Ofisi za TAKUKURU nchini. Yaelekeza Wakandarasi wasimamiwe kumaliza Ndani ya Muda.

Maelekezo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa ofisi nane za TAKUKURU iliyotoleqa
Mbele ya kamati na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete wakati wa zoezi la ukaguzi wa ofisi ya Mkoa wa Iringa. 

Akieleza mbele ya kamati , Ndg. Naibu Waziri Kikwete, ameeleza kuwa fedha zote zilizoelekezwa na Bunge kwa ajili ya miradi ya Maendeleo shilingi Bilioni 4.5 sawa na asilimia 100 za fedha zilizoombwa zimekwisha tolewa na ujenzi unaendeleaje katika ofisi za mikoa na wilaya mbalimbali nchini kama ilivyoelekezwa.

Mwenyekiti wa kamati , aliishukuru serikali kwa kufanikisha hili na kuomba uongozi wa wizara kuhakikisha wanasimamia majengo hayo yakamilike ndani ya muda uliopangwa.

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo