TANGAZO LA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA KAMPUNI YA ULINZI YA SHIMA
                                                                                        (SHIMA GUARD Co Ltd) TAREHE 09/11/2020
SHIMA GUARD – Ni Kampuni tanzu ya Shirika la Magereza linalotarajia kutoa nafasi za Ajira Ya Ulinzi hivi karibuni, ili uweze kuajiriwa na kampuni tajwa ni lazima uwe umepitia mafunzo yanayoendeshwa na kampuni hiyo bila malipo. Aidha, kampuni inatangaza nafasi za mafunzo hayo kwa wenye sifa zifuatazo:-
⦁ Awe raia wa Tanzania
⦁ Awe na umri wa miaka 20 - 50
⦁ Awe hajawahi kuhukumiwa au kuwa na rekodi ya makosa ya jinai
⦁ Awe na elimu ya kuanzia darasa la saba hadi kidato cha sita
⦁ Awe na tabia njema
⦁ Awe anajua kusoma na kuandika Kiswahili au Kingereza kwa ufasaha
⦁ Awe tayari kufanya kazi mahali popote atakapopangiwa mara baada ya kumaliza mafunzo
⦁ Awe hana rekodi ya matumizi ya dawa za kulevya
⦁ Awe na akili timamu
⦁ Asiwe na ulemavu wa aina yoyote

JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Barua ya maombi ya kujiunga na mafunzo ikiwa na namba ya simu ya muombaji itumwe kwa njia ya Posta kwa anuani ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Kampuni ya Ulinzi ya SHIMA (SHIMA GUARD Co. Ltd)
S.L.P 1176,
DODOMA.


Au kwa barua pepe ifuatayo:- This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Barua ya maombi itumwe ikiwa na viambatanisho vifuatavyo:-
⦁ Picha za Passport size mbili zilizopigwa hivi karibuni
⦁ Nakala ya cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria /Hakimu au kiapo (Affidavit original)
⦁ Nakala ya vyeti vya kuhitimu Elimu ya Msingi au Sekondari
⦁ Barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa/Kijiji sehemu anakoishi
⦁ Nakala ya kitambulisho chaTaifa (NIDA) au cha mpiga kura
⦁ Form ya uthibitisho wa afya yake kutoka Hospitali ya Serikali
⦁ Barua ya wadhamini wawili (02) wenye utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa /Kijiji zikiwa na picha mbili za wadhamini na namba zao za simu
N.B: Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 16/11/2020 na watakaokuwa na sifa watajulishwa

Imetolewa na,
Mkurugenzi Mtendaji,
Kampuni ya ulinzi ya SHIMA (SHIMA GUARD Co Ltd).